
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh Angelina Mabula
Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Mtathmini Mkuu wa Serikali kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo Bi. Evelyne Mugasha wakati akitangaza taratibu ambazo tayari serikali imeanza kuzichukua katika kuhakikisha wanamaliza migogoro ya ardhi nchini.
Akizungumzia suala la malalamiko ya wananchi ya fidia ya aridhi yanayotokana na ucheleweshwaji wa ulipaji wa fidia, Bi. Evelyne amesema tayari wizara hiyo imetunga sheria mpya ya uthamini na usajili ya wathamini ya mwaka 2016.