Ijumaa , 9th Sep , 2016

Licha ya kuanza vibaya kwa kupoteza mechi mbili katika ligi kuu Tanzania Bara ikiwa nyumbani, Klabu ya Mbao FC imesema ina imani kwamba itafanya vizuri mechi zijazo na kubaki katika ligi kuu.

Mbao FC

Baada ya kushindwa kufanya vyema kwenye mechi tatu za Ligi Kuu ya Tanzania Bara, uongozi wa klabu ya Mbao FC ya Ilemela kutoka jijini Mwanza umesema kwamba kikosi cha timu hiyo kinataraji kuanza safari siku ya Jumamosi kuelekea jijini Dar es Salaam kwa ajili ya pambano lao dhidi ya African Lyon.

Msemaji wa timu hiyo, Christian Malinzi amesema kwamba kwa sasa kocha mkuu wa klabu hiyo anajaribu kuyafanyia kazi mapungufu ambayo yameonekana kujitokeza hasa kwenye safu ya ulinzi.

Amesema kwamba licha ya kufungwa mechi mbili mfululizo tena wakiwa nyumbani bado wana amini watafanya vizuri msimu huu na kusalia katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara.