Ijumaa , 9th Sep , 2016

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu Emannuel Maganga, amezitaka mamlaka zinazohusika na watumishi wanaotuhumiwa kushirikaiana na wafanyabishara wa nchi jirani kuingiza mizigo kwa kukwepa kodi wachukuliwe hatua za kisheria haraka.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu Emannuel Maganga,

Brigedia Jenerali Mstaafu Magaga amesema maeneo ya mpakani kikiwemo kituo cha uhamiaji, polisi na kituo cha Mamlaka ya mapato cha Manyovu ni vituo muhimu vya kukusanya mapati hivyo uwepo wa watumishi wasio waadilifu unaathiri uchumi wa Taifa.

Amesema kuwa takwimu zinaonesha kuanzia mwezi Aprili hadi Septemba mwaka huu zaidi ya wahamiaji haramu 1,480 kutoka nchi jirani wamekamatwa wakijihusisha na shughuli mbalimbali za kiuchumi ikiwemo kufanya biashara bila kibali mkoani humo.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Uhamiaji mkoani Kigoma amesema msako wa kuwasaka wahamiaji hao mkoani humo ni endelevu kwa kuwa wengi wanajihusisha na matukio mbalimbali ya uhalifu pamoja na kufanya shughuli za kiuchumi bila kulipia kodi.