![](http://eatv.tv/sites/default/files/styles/detailpageimg/public/news/2016/07/29/muhongo..jpg?itok=C5n8-wIg×tamp=1473835055)
Waziri wa nishati na madini nchini Tanzania Prof: Sospeter Muhongo amewataka makatibu wakuu wa wizara kuhakikisha wanafanikisha mradi wa bomba la mafuta utakaotokea nchini Uganda kuja nchini Tanzania.
Akizungumza leo jijini Dar es salaam katika semina ya kuwaelekeza makatibu wakuu na wakuu wa mikoa ambao mradi huo utapita Prof. Muhongo amesema mradi huo ni wa gharama kubwa na unalenga kusaidia nchi hivyo ni sasa kwa makatibu wakuu hao kuonyesha ushirikiano ili kuufanikisha mradi huo.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Tanga ambaye ndiko mradi huo utaishia Bw. Martin Shigela amesema kupitia mradi huo wakazi wa mkoa wa Tanga watanufaika kwa kupata ajira zitakazotokana na ujenzi wake.
![](http://eatv.tv/sites/default/files/styles/detailpageimg/public/2016/07/29/56eac5a61ed4f.jpeg?itok=u2RWFQrd)