Jumanne , 11th Feb , 2025

Rais wa Marekani Donlad Trump ametangaza kuwa Marekani imedhamiria kununua na kumiliki Ukanda wa Gaza na kuhamisha Wapalestina milioni mbili wanaoishi huko, licha ya pendekezo hilo kupingwa vikali duniani.

Rais wa Marekani Donlad Trump ametangaza kuwa Marekani imedhamiria kununua na kumiliki Ukanda wa Gaza na kuhamisha Wapalestina milioni mbili wanaoishi huko, licha ya pendekezo hilo kupingwa vikali duniani.

Trump amewaambia wanahabari kuwa huenda akaruhusu mataifa ya kiarabu kuhusika katika kukarabati upya sehemu mbalimbali na kuwa atahakikisha raia wa Palestina wataishi maisha mazuri.

Mamlaka ya Palestina na kikundi kilicho na silaha cha Hamas ambao wamekuwa vitani kwa miezi 16 na Israel na kusababisha maafa Gaza, wamemjibu wakisema ardhi ya Palestina sio ya kuuzwa''.

Lakini waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameipigia upatu pendekezo hilo la Trump akilitaja ni ''mwamko mpya na bunifu''.

Haya yanajiri wiki tatu baada ya makubaliano ya kusitisha mapigano Gaza kuanza, Huku Hamas ikiachilia huru baadhi ya mateka wa Israel inayowazuia ili kubadilishana na Wafungwa wa Palestina walioko katika magereza ya Israel.

Wanajeshi wa Israel walianzisha kampeni ya kuvamia na kuharibu Gaza wakijibu shambulizi la kushtukizia la mwezi Oktoba tarehe 7 2023, ambapo watu 1,200 waliuawa na 251 wakatekwa nyara.

Zaidi ya watu 48,180 wameuliwa Gaza tangu mapigano hayo yaanze , hii ni kwa mujibu wa wizara ya afya inayosimamiwa na Hamas