Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Mhe. Seleman Jaffo,
Akizungumza Mkoani Iringa katika Halmashauri ya Mufindi ambapo anafanya ziara Mhe. Jaffo alitembelea mradi wa pampu ya kusambaza maji katika halmashauri hiyo mradi uliogharibu zaidi ya milioni 100.
Mhe. Jaffo amewataka watendaji kufanya kazi kwa weledi na kuwajali wananchi pamoja na fedha zinazotolewa na serikali kwa ajili ya miradi inayowafikia wananchi ili kutimiza lengo la serikali ya awamu ya tano ya kuiletea maendeleo nchi na wananchi kwa ujumla.
Waziri Jaffo pia alitembelea Zahanati ya Maduma, katika wilaya hiyo ambapo alikutana na Changamoto ya uchangavu wa majengo pamoja na kutokuwa na mashuka ya gonjwa jambo aliloliagiza kushughulikia kwa haraka sana kupata mashuka hayo huku wakiendelea kukarabati miundombinu mingine.
Wakiongea Watendaji wa Halmashauri hiyo wamesema kuwa Zahanati hiyo imekua ikihudumia watu wengi zaidi hivyo wamemuomba Naibu Waziri huyo kutoa kibali cha kuipanua na kuwa kituo cha Afya ili kuweze kutoa huduma kwa watu wengi zaidi.