Mkazi akichota maji ya Mto ambayo yanaweza kuwa sio safi wala Salama
Hayo yamebainishwa na Mtaalamu wa Ikolojia ya Bakteria kutoka Chuo cha Brighton, Profesa Huw Taylor wakati akizungumzia mradi wa shirika la Umoja la taifa la elimu,Sayansi na Utamuduni(UNESCO),na kuweka mfumo mpya wa udhibiti wa menejimenti ya majitaka(GWPP).
Amesema mpango wa dunia wa Maendeleo endelevu hauwezi kufanikiwa kama tishio la maji taka litaendelea kuwapo na lazima binadamu aendelee kujipanga kuhakikisha kwamba anatawala mazingira ya Maji.
Akizungumza katika Kongamano lilioandaliwa mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa wizara ya Maji na Umwagiliaji, Mbogo Futakamba amesema kongamano hilo lililenga kujadili kwa kina matatizo ya bakteria wanaosababisha magonjwa katika maji na madhara yake.