Katibu Mkuu wa UNCTAD Dkt. Mukhisa Kituyi
Akizungumza mjini Nairobi, Kenya kunakotarajiwa kuanza mkutano wa 14 wa kamati hiyo,Katibu Mkuu wa UNCTAD Dkt. Mukhisa Kituyi ametolea mfano uwezeshaji wanawake wajasiriamali wa mboga za majani nchini Tanzania kuweza kuuza bidhaa hizo kwenye hoteli za kitalii.
Dkt. Kituyi amesema kuwa kwa mda mrefu Tanzania ilikua inaagiza mbogamboga kutoka Kenya hivyo watawezesha wanwake wajasiriamali kutoka nchini Tanzania wanaofanyabishara ya kilimo cha mbogamboga kuwezeka kulima mboga za kiwango na kutosheleza soko la kwa ujumla.
Ametaja hatua nyingine ni kuhakikisha wanawake wanashiriki kwenye mikutano na kuwasilisha mada ambapo kwenye mkutano huo kutakua na mada maalumu ya jinsi ya kuhamisisha Wanawake katika biashara Kimataifa.