Jumatano , 29th Jun , 2016

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wakuu wa wilaya walioteuliwa hivi karibuni kusimamia miradi ya maendeleo katika maeneo yao ili waweze kumuwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika maeneo yao.

‘’Suala la ziara kwenye maeneo yenu ni jambo muhimu lazima muende vijijini mkawasikilize wananchi na kutatua kero zao’’ Amesema Majaliwa.

Pia mkatatue migogoro ya ardhi ambayo imeshamiri katika maeneo mengi nchini lakini kikubwa bunge linalomalizika fedha zitaanza kuja kwenye maeneo yenu hakikisheni mnazisimamia ipasavyo.

Akizungumza baada ya kula kiapo mtangazaji Godwin Gondwe amesema kwamba ataenda kuwatumikia wananchi wa Handeni na kuteuliwa nafasi hiyo ni heshima kubwa sana kwa wanahabari hivyo harta waangusha wananchi na wanahabari wenzake.