Jumatatu , 27th Jun , 2016

Serikali imetoa miongozo wa namna ya ujenzi wa majengo ya shule za msingi na sekondari pamoja na utengenezaji na ununuzi wa samani, ili kuhakikisha kuwa miundombinu inaboreshwa kukidhi mahitaji ya wanafunzi wenye ulemavu.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Mhandisi Stela Manyanya

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Mhandisi Stela Manyanya amesema hayo leo bungeni Mjini Dodoma na kuongeza kuwa wataendelea kuhamasisha ujenzi wa mabweni kwa ajili ya kuandikisha wanafunzi wengi wenye ulemavu ili kuwapunguziza adha ya kutembea umbali mrefu zaidi kufuata shule.

Mhandisi Manyanya ameongeza kuwa serikali inaendelea kutoa mafunzo maalumu kwa walimu katika ngazi mbalimbali ili kukabiliana na changamoto ya upungufu wa walimu katika eneo hilo.

Aidha, Naibu waziri huyo amesema kuwa serikali imeendelea kutenga fedha kwa ajili ya kununua na kusambaza vifaa vya kielimu na visaidizi kwa ajili ya wanafunzi wenye ulemavu wanaosoma katika shule za msingi na sekondari nchini.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Mhandisi Stela Manyanya