
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Beatrice Singanno amesema, mpango huo unasaidi kuendelea kukuza soka la vijana hapa nchini ambao hapo baadaye huweza kuwa wachezaji wakubwa ambao wataitangaza nchi katika ramani ya soka.
Beatrice amewataka wazazi kuwapa nafasi watoto kuweza kushiriki mashindano hayo ambayo huwasaidia kwa asilimia kubwa kwa kuweza kuwapatia hata ajira kwani michezo ni ajira kwa pia.
Beatrice amesema, Airtel inasaidia kuwapa fursa mbalimbali watoto ambao hujitokeza katika michezo ambao hata hivi sasa wanajivunia vipaji ambavyo vinaendelea kufanya vizuri kwa ndani na nje ya nchi.