Ijumaa , 14th Nov , 2025

Rais Samia Suluhu Hassan ameweka wazi kuwa uteuzi wa Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba umepitia ushindani mkubwa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa jukumu alilopewa Waziri Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba ni zito.

Akizungumza leo Novemba 14 mara baada ya kumwapisha Dkt. Nchemba kuwa Waziri Mkuu, Rais samia amesema vishawishi ni vingi lakini ana imani naye kutokana na ahadi aliyoitoa jana mara baada ya kuteuliwa kuteuliwa na kuidhinishwa rasmi na Bunge kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Amesema kuwa kwa umri wake Dkt. Chemba kazi itakuwa ni nzito lakini ana imani naye.

Baada ya kuteuliwa na kuidhinishwa rasmi na Bunge kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jana Novemba 13,2025, Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba amekula kiapo rasmi cha kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Novemba 14 katika Ikulu ya Chamwino, Dodoma.

Mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan na Viongozi wengine wa Serikali, Dkt Chemba ameapa kuwa atahudumu katika nafasi hiyo kwa uaminifu , nafasi atakayoishilikia kwa kipindi cha mwaka 2025 hadi 2030.