Mshambuliaji wa Azam FC, Didier Kavumbagu
Taarifa za ndani ya Mbeya City zinasema kwa asilimia kubwa, Kavumbagu raia wa Burundi na Mbeya City wameenda vizuri katika mazungumzo yao na wanaweza kumsajili kwa ajili ya kukitumikia kikosi hicho muda wowote kuanzia sasa.
Afisa Mtendaji wa Azam FC Saad Kawemba amesema hawana tatizo iwapo kama Mbeya City na Kavumbagu watakuwa wamemalizana kwani Kavumbagu amebakisha siku chache kumaliza mkataba wake ndani ya klabu ya Azam FC.