Jumanne , 7th Jun , 2016

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda, amewaagiza watendaji wa Kata, Wenyeviti wa serikali za Mitaa, pamoja na maofisa wa polisi, kuwafichua watu wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu ikiwa ni pamoja na orodha ya watu wanaoishi katika mitaa yao.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Felix Ntibenda.

Mkuu huyo wa Mkoa ametoa agizo hilo wakati akizungumza na viongozi hao kutoka katika maeneo mbalimbali ya jiji la Arusha, kwa lengo la kupanga mikakati ya kuimarisha ulinzi shirikishi.

Ntebinda amesema kuwa viongozi hao wa usalama wanatakiwa kuongeza nguvu katika ukaguzi wa wageni wanaofikia katika mahoteli ikiwa ni pamoja na kukagua mizigo wanayoingia nayo lakini na kujisajili kwa majina yao sahihi ili kupata mwanzo wa kuanzia pindi tukio lolote linapotokea.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Kamishna wa Polisi, Charles Mkumbo, amewataka watendaji hao kuwa na majina sahihi ya wakazi wa maeneo yao kwa kuandika kwenye madaftari ili kudhibiti uhalifu kabla haujatokea.

Nao vingozi hao wa usalama wameliomba jeshi la Polisi kuwa na usiri pindi wanapotoa taarifa ili waweze kuwafichua wahalifu bila kuwa na woga.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Felix Ntibenda