Ijumaa , 25th Apr , 2014

Jumuiya ya Uamsho na mihadhara ya kiisilam mjini Zanzibar imewataka viongozi wa kisiasa kuacha kuchanganya masuala ya kisiasa na kidini kwa kuwa kufanya hivyo ni kutaka kuvuruga amani ya nchi.

Kiongozi wa jumuiya ya Uamsho akiwa katika moja ya mikutano ya hadhara ya jumuiya hiyo kisiwani Zanzibar.

Wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, viongozi wa jumuiya hiyo Bw. Maalim Yusuph Hamis na bw. Said Amour Salim pia wamekanusha taarifa zinazoenezwa kwamba jumuiya hiyo ina mahusiano na chama cha wananchi CUF.

Wamemtaka mwenyekiti wa bunge maalum la katiba kuwachukulia hatua viongozi ambao wanahusisha suala la mchakato wa katiba na dini kwa kuwa kufanya hivyo ni kuwachanganya wananchi.