Alhamisi , 2nd Jun , 2016

Serikali ya Tanzania imesema kuwa ucheleweshaji wa mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu katika baadhi ya vyuo umetokana na kufanyika uhakiki wa wanafunzi kwa kuwa na uwepo wa wanafunzi hewa ambao wananufaika na mikopo hiyo.

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Naibu Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Selemani Jaffo.

Akiongea Bungeni leo Mjini Dodoma kwa Niaba ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Naibu Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Selemani Jaffo amesema kuwa Serikali imekua ikoboresha utoaji wa mikopo ila changamoto zilizojitokeza sasa ni pamoja na uwepo wa wanafunzi hewa.

Mhe. Jaffo amesema mpaka sasa serikali imeshapeleka fedha katika vyuo mbalimbali nchini isipokuwa baadhi ya vyuo ambavyo bado wanavifanyia uhakikia kikiwemo cha UDOM.

Mhe. Jaffo amesema kuwa kuwa baadhi ya wanasiasa wanalichukulia suala la mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya kisiasa wakati ukweli ni kwamba juhudi zinaonekana dhahiri kwa serikali kuongeza bajati kutoka shilingi bilioni 56 mwaka 2006-207 mpaka shilingi bilioni 473.