Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akiwa na balozi wa Oman nchini anaemaliza muda wake Bw. Saud Ali Mohammed Al Ruqaish.
Mhe. Samia amesema hayo jana alipokutana na balozi wa Oman nchini anaemaliza muda wake Bw. Saud Ali Mohammed Al Ruqaish, alipokwenda ofisini kwake kwa ajili ya kuaga.
Makamu wa rais ametumia nafasi hiyo kuiomba serikali ya Oman kuangalia uwezekano wa uwekezaji katika sekta za kilimo na biashara ambako kuna fursa nyingi za uwekezaji.
Aidha, amesema kuwa serikali ya Oman imekua na uhusiano na serikali ya Tanzania katika kukuza nyanja tofauti ambapo nchi hiyo imesaidia ujenzi wa chuo cha Afya.