Jumatatu , 18th Apr , 2016

Serikali imesema kuwa inaandaa viwango vya tozo za nauli za kuvuka katika daraja la Kigamboni.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia ujenzi Mhandisi Joseph Nyamhanga na kuongeza kuwa kwa hivi sasa watu watakuwa wanavuka bila tozo zozote. .

Mhandisi Nyamhanga amesema kuwa watembea kwa miguu na waendesha baiskeli watavuka bure bila ya kuwepo tozo zozote ili kuweza kuwapa fursa wananchi wa vipato vyote waweze kufurahia huduma ya usafiri katika daraja hilo.

Aidha vyombo vingine vya usafiri kama mikokoteni na maguta hayataruhusiwa kabisa kuvuka katika daraja hilo kwasababu za kiusalama zinazosababishwa na kutokuwepo kwa njia inayowaruhusu wao kupita.