Dkt. Mohammed Mang’una-Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Hayo yamesemwa na Mganga mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Daktari Mohammed Mang’una wakati anaongea na EATV ikiwa Leo ni siku ya Uzazi wa mpango duniani.
“P2 ni salama kabisa endapo itatumika kwa dharura na sio kutumia Kama njia ya Uzazi wa mpango ni kiuhalisia ina madhara makubwa ikitumika kiholela inaweza kubadili mzunguko wa hedhi lakini mbaya zaidi inaweza kuleta ugumba kwa mtumiaji, kwahiyo tunashauri Kama haupo tayari kubeba mimba ni vema ukaenda kwenye kituo cha kutolea huduma za Afya kwa ajili ya ushauri na njia sahihi ya matumizi ya Uzazi wa mpango”, alisema Dkt. Mohammed Mang’una-Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Kwanini kuna umuhimu wa kutumia Uzazi wa mpango?
“Lengo letu kufikia 2030 tuweze kupunguza vifo Vya mama na mtoto ambavyo wakati mwingine hutokea kwa sababu ya kutotumia Uzazi wa mpango lakini pia Elimu sahihi ya matumizi ya njia ya uzazi wa mpango na kuwafikia wananchi wote”,alisema Dkt.Warren Bright, Meneja Mawasiliano UNFPA.
“Uzazi wa mpango una faida kubwa kwa sababu unakuwa unajiandaa kwa ajili ya malezi lakini pia unaandaa Afya ya mzazi kabla ya kupata mtoto”, alisema Dkt.Katanta Simwanza, Meneja Mradi Afya ya uzazi na jinsia.
Je, vijana wana uelewa gani kuhusu matumizi ya uzazi wa mpango?
“Binafsi nafahamu kwa sababu toka nikiwa Primary nimekuwa nikijifunza na hiyo imenisaidia sana kwa sababu nimemaliza masomo yangu bila kupata changamoto ya mimba za utotoni “, alisema Getrude Clement, Kijana.
“Mimi naona elimu bado nashauri elimu iongezeke ikiwezekana vituo Vya kutolea huduma za Afya viwe na muda wa ziada ili wanafunzi wapate muda wa kupata elimu sahihi ya uzazi lakini pia vituo visogeswe karibu na mashule ili kundi la vijana liweze kufikiwa kirahisi”, alisema Rahim Naser, Kijana.