Jumamosi , 28th Sep , 2024

Wadau na wasimamizi wa uchaguzi nchini wametakiwa kuhakikisha uchaguzi ujao wa serikali za mitaa unaakisi 4R zilizoasisiwa na Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ikiwa ni pamoja na kushirikisha makundi tofauti katika jamii

Wadau na wasimamizi wa uchaguzi nchini wametakiwa kuhakikisha uchaguzi ujao wa serikali za mitaa unaakisi 4R zilizoasisiwa na Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ikiwa ni pamoja na kushirikisha makundi tofauti katika jamii

Rai hiyo imetolewa na msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, Dkt. Semistatus H. Mashimba uchaguzi katika wilaya hiyo na maeneo mengine lazima ushirikishe makundi mbalimbali ili kuepusha malalamiko ya wadau

Dkt. Semistatus amesema hayo katika Ofisi za Makao Makuu ya Halmashauri hiyo eneo la Nyamnyusi wakati akizungumza na viongozi wa vyama vya siasa, viongozi wa dini, wazee maarufu, vyama vya wafugaji na wakulima na watendaji wa vijiji na kata 

“Kampeni zitaanza tarehe 20 hadi 26 Novemba 2024 na uchaguzi utakuwa Novemba 27 mwaka huu kwahiyo tuwaombe vyama vya siasa,viongozi wa dini na wadau wote mliopo hapa tunaomba kipindi hiki kiwe na utulivu na amani kubwa tofauti na mazingira mengine,” amesema.

Naye Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kasulu, Abdallah Kazikwa   ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la Mkazi ambalo ni tofauti na zoezi lililopita la uandikishwaji katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura ili waweze kuitumia haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi wanaowafaa

Kwa upande wao viongozi wa vyama rafiki Wilaya ya Kasulu   wameipongeza Kamati ya Uchaguzi kwa kuwashirikisha katika tukio hilo muhimu huku wakibainisha  kuwa na imani nayo pamojana kutoa ahadi    kuipa ushirikiano pale  uatakapohitajika.

Katika hatua nyingine Katibu wa Baraza la Machifu Mkoa wa Kigoma,Abel Bussa ametoa rai kwa kila mwananchi mwenye sifa kujitokeza kugombea pamoja na kutoa ahadi ya kwenda kufundisha aliyojifunza leo kwa wengine juu ya umuhimu wa kupiga kura.