Ijumaa , 15th Apr , 2016

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ,Mhe William Lukuvi, amesema kuwa mikopo inayotolewa kwa matumizi ya ardhi lazima ziende katika kuendeleza kilimo ili kuhakikisha uchumi unakua kupitia sekta hiyo.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ,Mhe William Lukuvi.

Akiongea na wadau wa Taasisi za Fedha Mhe. Lukuvi amesema sasa watu waache kutumia ardhi kama dhamana ya kufanyia biashara pekee amesema sasa watu watalie mkazo madhumuni ya mikopo hiyo katika uendelezaji wa kilimo.

Lukuvi amesema endapo watu watawekeza kwenye kilimo kutaongeza ajira kwa kiasi kikubwa pia kinaweza kuliingiza taifa fedha za kigeni na kusema watu waache kuchukua fedha na kufanya biashara ya kununua na kuuza tu

Aidha katika hatua nyingine Waziri Lukuvi amezitaka taasisi za fedha kuheshimu hati miliki za kimila ambazo ni halali kisheria ili kuhakikisha wananchi wote wanapata mikopo itakayowasaidia kujikwamua kiuchumi.

Mhe. Lukuvi ameyataka mabenki yabadilishe udhamini wao kwenye masuala ya starehe kwa kuaandaa matamasha badala yake waongeze kipato cha mikopo kwa wananchi ili mabenki hayo yajivunie kwa kuweza kukuza uchumi wa wananchi hasa masikini wanaomiliki ardhi.

Kwa upande wao wadau wa mabenki hayo wamewataka wakulima wabadilike kutoka kwenye mfumo wa kukalia mashamba yao bila kuyaendeleza na sasa watumie nafasi hiyo kuendeleza kilimo chenye tija kwa manufaa yao na nchi kwa ujumla.

Sauti ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ,Mhe William Lukuvi,