Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa
Mkurugenzi Mkuu wa ofisi ya Taifa ya takwimu nchini Tanzania Dkt. Albina Chuwa amesema mara baada ya kupitishwa kwa ajenda hiyo, waliitisha kikao cha wadau wanaozalisha na kutumia takwimu ili kuelezea mwelekeo unaotakiwa.
Dkt. Chuwa amesema kuwa kwa sasa serikali ipo katika muundo wa kufuatilia utaratibu ambapo baada ya hapo watapelekea miongozi ya kwa makatibu wakuu ili waweze kugawana majukukumu katika takwimu hizo.
Na kuhusu takwimu na mabadiliko ya tabianchi kwa mujibu wa ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa iliyowasilishwa kwenye mkutano huo Dokta Chuwa amesema mfumo mzima wa ukusanyaji wa takwimu za mabadiliko ya tabia nchi utakamilika mwaka huu.
Ameongeza kuwa baada ya mwaka huu watakua na mahali pa kupatia muongozo na wahisani watakua tayari kusaidia uwezo wa kupambana na thari zinazotokana na mabadiliko ya tabia nchini.