Celine Dion akiwa na aliyekuwa mume wake Rene Angelil
Bw. Angelil waliooana na Dion mwaka 1994 na kufanikiwa kupata watoto watatu, amefariki dunia asubuhi Jijini Las Vegas kwa ugonjwa wa saratani.
Mwanamuziki Celione Dion alilazimika kupumzika mara mbili muziki baada ya mumewe Angelil kubainika kuwa anasumbuliwa na tatizo la saratani ya koo mwaka 2000.
Marehemu Angelil alizaliwa Montreal mwaka 1942, Baada ya kumiliki makundi ya muziki Canada alifuatwa na wazazi wake Dion ili kusaidia kuwa meneja wake tangu akiwa na umri wa miaka 12.