Mkuu wa Wilaya ya Mkinga,ambae ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama Mboni Mgaza.
Uharibifu huo unafanywa na wafanyabiashara wa Tanzania kwa kushirikiana na wafanyabiashra kutoka Kenya kwa miti aina ya Mikarambati na Mikoko wilayani Mkinga.
Akiongelea uharibifu huo Afisa Misitu wa Wilaya hiyo Frank Chambo amesema miti ya mikoko imekuwa ikikatwa kwa ajili ya nishati huku Mikarambati ikitumiwa kwa ajili ya kuchonga vinyago na wafanyabiashara kutoka Kenya.
Akizungumza wilayani Mkinga baada ya operesheni iliyofanywa awali kufanikiwa lakini baadhi ya wahamiaji kutoka nchi jirani ya kenya wameanza kuingia kupitia njia za majini na njia za panya mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama Mboni Mgaza amesema hatua hiyo inafuatia misitu ya hifadhi kuharibiwa vibaya katika baadhi ya maeneo na kupoteza uoto wa asili.