
Mkurugezi wa Habari na Mawasiliano CUF Bw. Ismail Jusa Ladhu
Akiongea leo Jijini Dar es Salaam Mkurugezi wa Habari na Mawasiliano CUF Bw. Ismail Jusa Ladhu amesema taarifa hizo ni za uongo na kuwataka Watanzania wazipuuzie kwa kuwa Maalim Seif ni mzima wa afya.
Jusa amevitaka vyombo vya sheria viweze kufatilia suala hilo ili sheria iweze kuchukua mkondo wake kwa kuwa habari hizo zinaasharia uchochezi na kuvuruga amani.
Aidha Mh. Jusa ameizungumzia hali ya kisia ya Zanzibar na kusema bado zinahitajika juhudi za makusudi kutatua mgogoro huo huku akimuomba rais Dkt. John Magufuli kuweza kuingilia kati suala hilo.