Naj
Naj ambaye amekuwa katika game ya Bongo Fleva kwa miaka kadhaa sasa, amesema kuwa ameshuhudia wasanii wengi kutokuendelea na wala kubadilika kutokana na kubweteka na kutumia vibaya kile wanachikipata kutoka katika muziki.
Staa huyo ambaye anatamba sasa na rekodi ya No Going Home, pia akagusia kazi zake akieleza, baada ya kazi hii, anatarajia kufunga mwaka na kazi nyingine mpya, akiwataka mashabiki wake kufahamu kuwa, ujio wake wa sasa hautakuwa na nafasi ya ukimya tena.