
Mwenyekiti wa CHANETA Anna Kibira amesema, wachezaji hao baadaye watakuwa tegemeo kwa timu ya Taifa.
Kibira amesema, wachezaji wengi walio timu ya taifa umri wao ni mkubwa na wanatakiwa kuandaa vijana ambao watakuja kushika nafasi zao.
Kibira amesema, iwapo mikakati ya kusaka vijana chipukizi itaanza sasa hivi kuna uwezekano mkubwa Taifa Queens ya mwakani ikawa na wachezaji wenye damu changa na kiu ya mafanikio.
Kibira amesema, CHANETA watakuwa sambamba na wanachama hao katika kuhakikisha malengo yao yanakamilika kwa asilimia kubwa.