Jumanne , 29th Sep , 2015

Rapa Witnesz a.k.a Kibonge Mwepesi ambaye kando ya muziki hivi sasa anajihusisha na kusaidia watu wenye unene kupungua, ametolea ufafanuzi namna ambavyo anakabiliana na shughuli hiyo, wakati yeye binafsi akiwa na umbo lenye unene na uzito mkubwa.

Rapa Witnesz a.k.a Kibonge Mwepesi

Witnesz amesema kuwa, sio mara zote kitu ambacho mtu anakifanya kama kazi kikaweza kikajionesha kwake binafsi, huku akijitetea kuwa kuna tofauti kubwa katika mwili wake wa zamani na wa sasa, kitu ambacho eNewz tunawaachia kazi mashabiki kuamua.

Kuhusiana na suala hilo, Witnesz mwenyewe hapa akiwa na sababu lukuki za kujiamini, anaeleza.