Naibu Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na watoto Mhe. Pindi Chana
Akiongea Jijini Dar es Salaam, katika mkutano wa kujadili namna ya kukabiliana na ukatili kwa watoto Naibu Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na watoto Mhe. Pindi Chana amesema ukaguzi wa mazingira pamoja na kuvifanyia usafi vyoo vinavyotumiwa na watoto mashuleni ni haki ya msingi ya kutasaidia kuondokana na uwezekano wa watoto kupata magonjwa ikiwa ni pamoja na kipindupindu.
Mh. Chana amesema kuwa watoto wengi wapo katika hatari ya kuugua ugonjwa huo kutokana na shule nyingi kukosa huduma nzuri za kiafya ikiwemo choo,, Maji safi na Salama na menginye.
Mhe. Pindi Chana amesema tafiti zinaonesha kuwa ukatili wa kijinsia kwa watoto unahusiana na ongezeko la hatari ya kupata matatizo ya afya ya uzazi, pamoja na maambukizi ya magonjwa ya UKIMWI pamoja na magonjwa mengine ya zinaa.

