Jumatatu , 22nd Jun , 2015

Serikali imewataka wananchi wajitokeza kwa wakati kujiandikisha katika Daftari la kudumu la mpiga kura kwa mfumo wa BVR na wazingatie muda uliowekwa na Tume kwa kuwa hakutakuwa na uandikishaji mwingine baada ya zoezi hilo kupita.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Uratibu na Bunge Mh. Jenista Muhagama.

Akiongea leo Bungeni katika Kipindi cha Maswali na Majibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Uratibu na Bunge Mh. Jenista uhagama amesema kuwa Tume itaongeza muda kulingana na muitikio wa watu katika eneo husika ila muda utakaongezwa ukipita na watu wakiwa hawapo vituoni tume itafunga vituo hivyo.

Mh. Mhagama amesema kuwa serikali inaelwa kuwa muamko wa wananchi kujiandikisha ni mkubwa lakini amewataka wananchi waendelee kujitokeza kwa wingi zaidi ili kuweza kupata haki yao ya Msingi ya Kidemkrasia.

Mh. Mhagama wananchi wanaoendelea na shughuli zao wakati wamesikia kuwa Dafari lipo katika maeneo yao wasitegemee kama zoezi hilo litarudi tena katika maeneo hayo hivyo kujitokeza kwa wakati jambo ambalo watanzania wanatakiwa kuzingatia.

Kauli hiyo ya serikali imekuja baada ya Mbunge Masoud Abdallah Salim kudai kuwa kuna wananchi wanalalamika kukosa kujiandikisha katika maeneo ambayo uandikishaji huo tayari umeshafanyika.