Jumanne , 16th Jun , 2015

Msanii wa muziki M2TheP, ametumia nafasi yake kama kijana mwenye ushawishi katika jamii kuwashawishi vijana kujiandikisha kwa wingi na kushiriki katika suala zima la uchaguzi mwezi Oktoba mwaka huu.

M2THEP

Mkali huyo ambaye kwa sasa yupo katika matayarisho ya video ya ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina Tula chini ya Adam Juma, hapa anasisitiza mwenyewe kuwa vijana wanatakiwa kufahamu kuwa, ni mtu binafsi ndiye anayehusika katika kumchagua kiongozi wake na si kuchaguliwa na wengine.

Kwa maneno haya stra huyu anaungana moja kwa moja na kampeni tunayoiendesha ya Zamu Yako 2015 kukusisitiza kijana kuhakikisha kuwa anashiriki katika uchaguzi mwaka huu.