
Akizungumza na East Africa Radio, kuhusiana na matokeo mabaya yanayoendelea kupatikana katika mechi mbalimbali za Timu ya Taifa Taifa Stars Mkwasa amesema, kwa mwenendo huu Tanzania inazidi kudhalilika kwani badala ya kwenda mbele katika soka tunazidi kurudi nyuma.
Mkwasa amesema, wasimamizi wa timu ya Taifa wanatakiwa kujenga timu upya na kutafuta watu wanaoweza kusimamia timu ikasimama na ikapata sapoti na kuzidi kusonga mbele.