Jumatatu , 20th Oct , 2025

Mgombea Urais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha wananchi CUF Gombo Samandito Gombo amesema atakapopata ridhaa ya kuwa Rais atafanya utaratibu wa kugawa ardhi ya Tanzania upya kwa wanaohitaji kwasababu ardhi ya Tanzania ni mali ya umma na kwamba sio mali ya watu wa

Mgombea Urais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha wananchi CUF Gombo Samandito Gombo amesema atakapopata ridhaa ya kuwa Rais atafanya utaratibu wa kugawa ardhi ya Tanzania upya kwa wanaohitaji kwasababu ardhi ya Tanzania ni mali ya umma na kwamba sio mali ya watu wanaoiita ni mali ya  wawekezaji ambao wamekuwa wakichukua sehemu kubwa na kuwaacha wananchi wakikosa maeneo ya kufanyia shughuli zao za kilimo.

Mgombea urais Gombo ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro ikiwa ni muendelezo wa kampeni zake kuelekea uchaguzi mkuu mwaka huu ambapo amesema kwamba atahakikisha anagawa upya ardhi ya Tanzania.

"Mimi nikichaguliwa kuwa Rais nitafanya utaratibu wa kugawa ardhi ya Tanzania upya kwa wanaohitaji nitafanya hilo kwasababu ardhi ya Tanzania ni mali ya Umma sio mali ya watu wanaojiita wenyewe ni wawekezaji wanachukua mashamba makubwa watu wengine wanakosa sehemu ya makazi na kufanyoa shughuli zao za kilimo,"alisema Gombo.

"Mimi ardhi ya Tanzania nitafanya ugawaji upya ili kila mtu apate ardhi anayostahili kulima nitaigawa ardhi upya na bahati nzuri mimi ni mtaalamu wa mipango miji na vijiji ndio taaluma yangu niliyosomea hivi wanavyolalamika wananchi wa Rudewa kwamba hawana pa kulima lakini mashamba yapo mapori yapo wakiuliza wanaambiwa shamba la fulani ukiuliza unatajiwa watu wakubwa wakubwa tu mwisho wa siku tunakosa hata maeneo ya ufugaji,"alisisitiza Gombo.

Akiwa Dumila Mkoani humo mgombea urais Gombo alisimama na kusalimia wananchi wa eneo ikiwa ni pamoja na kutoa ahadi mbalimbali ikiwemo kuwafikishia huduma ya maji ipasavyo.