Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Prof. Ibrahim Lipumba amesema endapo atapata ridhaa kutoka Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) ataunda serikali ya Umoja wa Kitaifa pamoja na kusimamia maslahi ya wananchi.
Akiongea wakati wa kuchukua fomu za kuwania urais kupitia CUF, Prof. Lipumba amesema amejiwekea lengo la kuhakikisha kupitia umoja huo wa kitaifa utasaidia katika kuwaunganisha watanzania wote pamoja na kupiga vita suala zima la rushwa pamoja na kupitia mikataba yote ili nchi iweze kunufaika na rasilimali zilizopo.
Aidha Prof Lipumba ambaye leo amechukua fomu ya kuwania urais kwa tiketi ya chama cha CUF, amewata wananchi kujitokeza kwa wingi katika kujiandisha katika daftari la Kudumu la Wapigakura.
