Jumatatu , 16th Jan , 2023

Wachezaji 40 wa sanaa za mapigano wanatarajia kushiriki Ligi ya Fay herous ambayo itaanza Februari 25 mwaka huu kwenye fukwe ya Azura Dar Es Salaam.

Ligi hiyo imeandaliwa  na Chama cha Wushu(TWA)  Tanzania kwa kushirikiana na Kamisheni ya Kusimamia ngumi za Kulipwa Tanzania ( TPBRC) na Klabu ya Fay Herous .

Katibu Mkuu wa  TWA  Sensei Gola Kapipi ,alisema kuwa wachezaji hao ni WA michezo ya ngumi za Kulipwa ,kickboxing Judo ,Karate na Wushu.

"Ligi Hii itakuwa inafanyika kila mwezi na tunatoa Fursa  kwa michezo ambayo haifanyi mashindano  iweze kutoa nafasi ya Vijana kushiriki  waweze kujitengenezea kupata ajira na kuinua michezo hiyo," alisema Sensei Kapipi.

Naye Katibu Mkuu wa TPBRC  Yahya Poli,alisema kuwa kwa ngumi za Kulipwa itashirikisha mapambano tisa  kati ya hayo  yapo ya Wanawake.

'' lengo ni kukuza,kuibua na kuendeleza vipaji vya vijana kupitia mchezo huo''Katibu Mkuu wa TPBRC  Yahya Poli

Kwa upande wa Kaimu Mkuu wa Kitengo Cha Uhusiano na mawasiliano  wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT )  Najaha Bakari,aliwaomba wadau na wadhamini kujitokeza kuunga mkono kwa kusaidia kufanikisha Ligi hiyo.

'' Wito  mwingine kwa waandaji kuendelea kuandaa mashindano mengi Ili kutoa fursa kwa wachezaji kushiriki  na kuibua vipaji mtaani  Ili kuweza kupata wawakilishi bora  kimataifa.