Baadhi ya wanachama wa Simba wakishuhudia moja ya mechi za timu yao.
Zoezi la kupokea pingamizi kwa wagombea zaidi ya 41 wa nafasi mbalimbali za uongozi wa klabu ya simba katika uchaguzi mkuu wa klabu hiyo utakaofanyika june 29 mwaka huu limehitimishwa hii leo
Katibu mkuu msaidizi wa kamati ya uchaguzi ya klabu hiyo Khalid Kamguna amesema kuwa kila kitu kimekwenda vizuri huku akiwapongeza wanachama wa klabu hiyo kwa kuwa makini kwani mapingamizi safari hii yamekua machache japo katika zoezi hilo changamoto hazikukosekana
Kamguna amesema moja ya changamoto walizokabiliana nazo katika zoezi hilo ni pamoja na baadhi ya wanachama kutojua ni nani na kwanini anataka kumwekea pingamizi, pia baadhi yao kushindwa kutoa vielelezo vyao vya uthibitisho wa uanachama wao pamoja na vielelezo vya hoja za pingamizi walizoweka kwa wagombea.