Jumatano , 28th Mei , 2014

Kufuatia kumalizika kwa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2013-14, wadhamini wa ligi hiyo kampuni y

Tuzo mbali mbali ambazo zimetolewa kwa timu,waamuzi na wachezaji na makocha waliofanya vizuri msimu wa 2013-14 wa ligi kuu TZ Bara.

Kufuatia kumalizika kwa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2013-14, wadhamini wa ligi hiyo kampuni ya huduma za simu za mkononi VODACOM wametoa zawadi kwa washindi mbali mbali.

Bingwa wa ligi hiyo Azam FC wamepata zawadi ya fedha taslimu shilingi million 75, washindi wa pili Yanga wamepata shilingi milioni 35, washindi wa tatu Mbeya City wamepata shilingi milioni 26 na washindi wanne Simba wamepata shilingi milioni 21. Yanga SC pia imeibuka timu yenye nidhamu na kuzawadiwa Sh. Milioni 16 ikizipiku Azam FC na JKT Oljoro. Hii ni mara ya pili kwa Yanga kwani msimu uliopita pia walishinda tuzo hiyo. Yanga ilipata kadi nne tu za njano na hawakupata hata kadi moja nyekundu.

Kwa upande wa wachezaji, Kipre Tchetche wa Azam FC ameibuka mchezaji bora kwa kuwashinda Lugano Mwangama wa TZ Prisons na Anthony Matogolo wa Mbeya City. Kipre Tchetche amezawadiwa shilingi million 5.2 kwa ushindi huo.
Kipa wa Mtibwa Sukari ya Morogoro, Hussein Sharrif maarufu kama Casillas Munyama, ameshinda tuzo ya mlinda mlango bora na kujipatia shilingi million 5.2 akiwazidi David Burhan wa Mbeya City na Beno Kakolanya wa Prisons. Naye Amisi Tambwe wa simba amepata tuzo ya ufungaji bora na shi milioni 5.2. kwa mabao yake 19. Hata hivyo, hakukuwa na mchezaji hata mmoja kati ya walioshinda tuzo kutokana na wachezaji hao kuwa mapumzikoni baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu,

Juma Mwambusi wa Mbeya City, ameshinda tuzo ya kocha bora, akiwaangusha Charles Boniface Mkwasa wa Yanga SC na Mecky Mexime wa Mtibwa Sugar na kupewa Sh. Milioni 5.2. Lakini pia kocha huyo naye hakuwepo kwani kwa sasa yuko nchini Sudan na timu yake wakishiriki michuano ya bonde la mto Nile.

Kwa upande wa waamuzi, Israel Mujuni Nkongo wa Dar es Salaam ameibuka mwamuzi bora akijipatia Sh. milioni 7.8 kwa kuwazidi Isihaka Shirikisho wa Tanga na Jonasia Rukia wa Kagera.