Jumatatu , 20th Jul , 2020

Beki  na nahodha wa zamani wa Yanga Kelvin Yondani  ataikosa mechi  ya Yanga dhidi ya Mtibwa Sugar itayopigwa Jumatano hii katika uwanja wa  Jamhuri mkoani Morogoro kutokana na kuwa na matatizo ya kifamilia.

Kelvin Yondani

Kauli hiyo imetolewa  na Mkuu wa kitengo cha Habari na Mawasiliano, Hassani Bumbuli na kusema kuwa  ni kweli nyota huyo hatokuwa  miongoni mwa kikosi ambacho kinaondoka leo majira ya saa saba mchana  huku akiweka wazi kuwa  bado hajapata ratiba kamili ya wachezaji ambao watasafiri. 

''Malengo yetu msimu huu ilikuwa tuchukue  ubingwa lakini tumekosa  ndiyo maana tunapambana katika mechi zote zilizobakia tushinde kwaajili ya kujiweka katika mazingira mazuri ya kukaa nafasi ya pili'' amesema Bumbuli.  

Yanga sc itajitupa dimbani Jumatano ya wiki hii dhidi ya Mtibwa Sugar katika uwanja wa Jamhuri huku wakiwa na kumbukumbu ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 nyumbani na Mwadui fc ya shinyanga ilhali Mtibwa wakitoka kupokea kipigo cha bao 1-0 dhidi ya KMC katika uwanja wa nyumbani wa CCM Gairo mjini Morogoro.