
kiongozi huyo ameeleza kuwa anajua wanapoelekea ni pagumu zaidi ya walipotoka ndio maana wameamua kuwekeza mapema kwenye maandalizi ili kulipa nafasi benchi la ufundi kujenga timu ya ushindani.
“Malengo ya Yanga yalikuwa ni kufika robo fainali lakini kwa mwenendo wetu kwenye mechi za hatua ya makundi imetupa hamasa na kuona kama tunaweza kufika mbali zaidi ndio maana tumekusudia kuongeza ukaribu na benchi la ufundi ili kutekeleza mahitaji yao na kutuandalia timu ya ushindani itakayotupa tunachokitaka huko tunapoelekea,” amesema Rais wa Yanga, Eng.Hersi Said.
Kikosi cha Yanga kimeingia kambini leo kujiandaa na mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi dhidi ya TP Mazembe pamoja na mechi za Ligi Kuu na Kombe la FA
Mwisho.