Ijumaa , 13th Feb , 2015

Michuano ya Kombe la Shirikisho inaanza kutimua vumbi hapo kesho ambapo Yanga inakutana na BDF ya nchini Botswana, Mechi itakayochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Kikosi cha wachezaji wa timu ya Yanga

Akizungumza na East Africa Radio, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka nchini TFF, Celestine Mwesigwa amesema, utakuwa ni mchezo mzuri na kila mmoja kuona vilabu vya hapa nchini vinafanya vizuri kutokana na kiwango cha mpira hapa nchini kwa miaka ya nyuma vilikuwa sio vya kuridhisha.

Mwesigwa amesema, Shirikisho lina wajibu wa kuhakikisha timu zinaandaliwa ili ziweze kufanya vizuri pamoja na kuhakikisha mchezo unachezwa kwa kufuata sheria za TFF, CAF na FIFA.

Mwesingwa amesema, kutokana na CAF kubadili sheria za timu shiriki za kombe hilo, timu zote za hapa nchini zimehakikisha zinatimiza majukumu yote yanayohitajika katika kuhakikisha wanafanikisha ushiriki wa michuano hiyo.