Mshambuliaji wa TP Mazembe Mtanzania Thomas Ulimwengu.
Kikosi cha mabingwa mara tano wa soka barani Afrika, timu ya TP Mazembe ya DRC wanatarajiwa kutua nchini usiku wa leo tayari kwa mchezo wa Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji Yanga SC, utakaopigwa siku ya Jumanne katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
TP Mazembe ambayo anachezea Mtanzania Thomas Ulimwengu [Rambo] inakuja na kikosi cha wachezaji 18, akiwemo mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Emmanuel Ulimwengu.
Kikosi kamili kinachokuja na Mazembe ni; Robert Kidiaba, Sylvain Gbohou, Issama Mpeko, Joel Kimwaki, Thomas Ulimwengu, Christian Koume, Jean Kasusula, Salif Coullbaly, Merveille Bope, Jose Badibake, Kissi Boateng na Roger Assale.
Wengine ni Rainford Kalaba, Deo Kanda, Adama Traore, Chriastian Luyindama, Nathan Sinkala na Joas Sakuwaha.
Maofisa wa benchi la Ufundi wanaokuja ni Theobald Binamungu, Mohamed Kamwanya,Dony Kabongo, Frederic Kitengie na Andre Ntime.
Madaktari ni Hurbert Velud, Pamphile Mihayo, Mhudumu Richard Mubemb na Maofisa wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Heritier Yinduka, Arther Kikuni na Meshack Kayembe.
Kikosi hicho kinatarajiwa kuwasili saa 3:00 usiku na kesho jioni kitakuwa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam kwa mazoezi mepesi tayari kwa mchezo huo wa pili kwa kila timu baada ya awali Mazembe wao kushinda 3-1 katika mchezo wa kwanza nyumbani dhidi ya Medeama ya Ghana na Yanga kufungwa ugenini kwa bao 1-0 na MO Bejaia ya Algeria siku ya Jumapili iliyopita
Na kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na shirikisho la soka nchini Tanzania TFF ni kwamba waamuzi wa mchezo huo watakuwa ni Janny Sikazwe wa Zambia atakayepuliza filimbi, akisaidiwa na washika vibendera Jerson Emiliano Dos Santos wa Angola na Berhe O'michael wa Eritrea.