Jumamosi , 28th Mei , 2016

Baraza la Wazee la Klabu ya Yanga limelitaka Baraza la Michezo nchini (BMT) na Shirikisho la Soka nchini (TFF) kuiruhusu sekretarieti ya Yanga kuitisha mkutano mkuu wa dharura.

Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Yanga, Ibrahim Akilimali, amesema mkutano huo utakuwa ni wanachama wenye agenda moja ya uchaguzi ili wanachama hao wapewe taarifa kuhusu uchaguzi.

Akilimali amesema, Sekretarieti hiyo pia inatakiwa kuwaaarifu viongozi wa wizara, TFF, DRFA na wadau wengine wanaohusika ili kuweza kushuhudia maamuzi ya wanachama wa klabu ya Yanga.

Akilimali amewataka pia wanachama wa Yanga kuzingatia sheria za klabu kuelekea katika zoezi la uchaguzi wa viongozi wa klabu hiyo ili kuhakikisha hali ya amani na usalama inaendelea kuwa nzuri katika klabu hiyo.