Jumatatu , 12th Sep , 2016

Mswiss Stan Wawrinka, ametwaa taji la mashindano ya wazi ya Marekani, baada ya kumbwaga mchezaji namba moja kwa ubora duniani, Novak Djokovic, kwa set 6-7 (1-7) 6-4 7-5 6-3, usiku wa kuamkia leo, uliopigwa Flushing Meadows, New York.

Stan Wawrinka

Djokovic alipambana katika hatua za mwanzo, lakini alikuja kupatwa na uchovu kwenye raundi ya nne, na kujikuta akipoteza mchezo.

Taji hilo ni la kwanza kwa Wawrinka katika US Open, na ni la tatu kwake katika mataji makubwa ya tenesi (Grand Slam), baada ya kutwaa mataji ya wazi ya Australia, mwaka 2014, na taji la wazi la Ufaransa mwaka jana.