Jumapili , 6th Jul , 2025

Wazungu wanasema "Age is just a number" wakimaanisha Umri ni namba tu! ni msemo unaosisitiza miaka sio kigezo pekee cha uhai wa mtu,kumjaji,uwezo wake, akili,muonekano,mapenzi au kumtilia shaka sababu ya umri.

Kutoka kulia ni Kajala, Ray C na Tiwa Savage

Hawa ni baadhi ya mastaa wa kike na umri wao halisi kuanzia miaka 43 na kuendelea, lakini kimuonekano ni mabinti flani hivi wa miaka ya 2000 (Gen Z) au kama gari tunasema ni 'Plate Number F' yenye Zero Kilomita.

-Mariah Carey miaka 56, muimbaji na mwandishi wa nyimbo Marekani

-Jennifer Lopez maarufu kama J.LO miaka 55. Muimbaji,muigizaji, mfanyabiashara na dancer

-Taraj P Henson (54) Muigizaji mkongwe Marekani

-Shakira (48) Malkia wa muziki wa Latin duniani kutoka Colombia

-Tiwa Savage ana miaka 45, ni msanii wa muziki Nigeria

-Kelly Rowland (44) mwanamuziki Marekani

-Kajala Masanja miaka 43, muigizaji maarufu Tanzania

- Ray C nae 43 ni msanii wa kike wa BongoFlava