Shirikisho la Soka Afrika (Caf) limethibitisha majina hayo kuwa mwamuzi wa kati atakuwa Rédouane Jiyed akisaidiana na Mohamed Lahmidi na Hicham Ait Abbou.
Rédouane Jiyed atachezesha mchezo huo utakaopigwa Uwanja wa Essipong Sports jijini Sekondi, Ghana ambapo kila timu itahitaji ushindi wake wa kwanza baada ya michezo yao mitatu ya awali kutopata matokeo ya kuridhisha.
Katika mchezo wa awali uliopigwa Julai 16 mwaka huu Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Yanga ililazimishwa sare ya bao 1-1 na kubaki mkiani mwa Kundi A baada ya kufungwa katika michezo mingine miwili ya awali huku Medeama ikiwa nafasi ya tatu kwa kufungwa mechi moja na kutoa sare mbili.
MO Bejaia ya Algeria inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi tano huku vinara TP Mazembe ya DR Congo wakiwa wamejikusanyia pointi saba mpaka sasa.




