Jumatatu , 15th Sep , 2025

Jeshi la polisi pia limemweekeza Polepole kufika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai ili aweze kutoa maelezo kuhusiana na tuhuma hizo anazozitoa katika mitanzao ya kijamii.

Jeshi la Polisi Tanzania limesema kuwa limefungua jalada la uchunguzi na linaendelea kuchunguza tuhuma mbalimbali ambazo amekuwa akitoa aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Herson Polepole toka Julai 2025.

Taarifa ya jeshi ya polisi imesema kuwa tuhuma ambazo ameendelea kuzitoa Polepole kupitia mitandao ya kijamii zinaashiria uwepo wa makosa ya kijinai na kwa mujibu wa sheria zinahitaji ushahidi wa kuzithibitisha zitakapowasilishwa mahakamani.

Baada ya kufungua jalada na kuanza uchunguzi, Jeshi la Polisi mbali na kukusanya ushahidi limekuwa likifanya jitihada za kumpata Polepole ili aweze kutoa maelezo au ushahidi na vielelezo kuthibitisha tuhuma hizoili kuwezesha hatua nyingine za kisheria kuchukuliwa.

Jeshi la polisi pia limemweekeza Polepole kufika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai ili aweze kutoa maelezo kuhusiana na tuhuma hizo anazozitoa katika mitanzao ya kijamii.