Jumatatu , 7th Dec , 2015

Wachezaji wa Simba waliokuwa katika kambi ya timu ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars wameungana na wenzao mjini Zanzibar ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Ligi Kuu Bara inayotarajiwa kuendelea Desemba 12 ambapo itaanza kazi na Azam FC.

Said Ndemla, Hassan Isihaka na Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ ndiyo wachezaji waliokuwa katika kikosi cha Tanzania Bara kilichoshiriki michuano ya Chalenji na kutolewa katika hatua ya robo fainali isipokuwa Waganda wawili, Hamisi Kiiza na Juuko Murshid ambao bado hawajaungana na kikosi hicho.

Ibrahim Ajibu tayari alijiunga na kikosi cha Simba mapema kwa kuwa hakwenda Ethiopia ilipofanyika michuano ya Chalenji baada ya timu kuondoka na kumuacha ambapo awali hakupewa maelezo, lakini baadaye akatakiwa kwenda Ethiopia, lakini hakaueleza uongozi wa TFF hakuwa jijini Dar es Salaam.