Katibu Mkuu wa BFT Makore Mashaga amesema, mabondia wanaounda timu za Taifa hawataziwakilisha Klabu zao katika mashindano hayo na badala yake watashiriki wakiwa mabondia wa timu ya Taifa.
Mashaga amesema, wamepanga kuyatumia mashindano hayo kwa ajili ya kuboresha timu ya taifa itakayokwenda nchini Cameroon kutafuta viwango vya kufuzu kucheza Olimpiki RIO 2016.
Mashaga amesema, hawana mpango wa kuvunja timu ya Taifa wakati wa mashindano hayo badala yake wataiboresha kwa kuiongeza mabondia wengine watakaoonyesha kiwango kizuri.
Mashaga amesema, katika mashindano hayo timu za mikoa ya Tabora, Mwanza, Kigoma, Kagera na Temeke zimethibitisha kushiriki mashindano hayo.