Alhamisi , 14th Apr , 2016

Baada ya Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, kukakibidhi ulingo wa masumbwi kwa Jeshi la Wananchi Tanzania JWTZ wiki iliyopita, Jeshi hilo limetoa ruhusa kwa vyama vya mchezo huo kuutumia ulingo huo muda wowote inapohitajika.

Mkuu wa kurugenzi ya michezo Jeshini, Meja Jenerali Issa Nasoro, amesema wanatoa ulingo huo kwa wanamichezo ili kusaidia mchezo wa masumbwi upate kukua na kutoa mabondia wazuri watakaoiletea heshima nchi.

Meja Nasoro amesema Jeshi linautunza ulingo huo ili udumu kwa muda mrefu na pindi ukihitajika utatolewa na ukishatumika utarejeshwa jeshini.

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Nape Moses Nnauye, ndiye aliyekabidhi ulingo huo wiki iliyopita kwenye hafla iliyofanyika ukumbi wa Jeshi,msasani jijini Dar es Salaam.