
Kushoto ni Haji Manara na kulia ni kocha msaidizi wa Simba
Manara amesema kocha huyo bado yupo Msimbazi na taarifa hizo si za kweli kwani timu ipo kwenye hali zuri na benchi la ufundi lina maelewano ya hali ya juu tofauti na ilivyoandikwa kuwa Masoud na kocha mkuu Patrick Aussems hawaelewani.
"Leo nimepigiwa simu nyingi toka kwa waandishi wa habari na washabiki wa Simba kutaka kujua ukweli wa taarifa zilizoandikwa kwenye gazeti moja likidai kocha msaidizi wa Simba anaondoka baada ya kutofautiana na kocha Mkuu Patrick Aussems" amesema Manara.
''Nawaambia Simba ni shwari na kilichoandikwa ni hekaya na hadithi, tusitolewe mchezoni kirahisi rahisi, tuendelee kuwa wamoja na tusiyumbishwe kwa maneno ya mahotelini'', ameandika Manara.
Kwa upande mwingine Simba leo inaingia uwanjani majira ya saa 12:00 jioni kucheza mchezo wake wa pili wa ligi kuu soka Tanzania Bara dhidi ya Mbeya City utakaopigwa kwenye uwanja wa taifa. Simba inaingia uwanjani bila ya mfungaji wake bora wa msimu uliopita Emmanuel Okwi ambaye anasumbuliwa na maumivu ya mgongo.